Elinewinga Family
.
img img

1).Elikyesia - Kuzaliwa.

Historia ya Bibi Elikyesia.Bibi Elikyesia Nsero Salema Kileo alizaliwa mwaka 1890 akiwa mtoto wa kwanza wa Nsero Salema Kileo.Nsero alikuwa na wake wawili, Elikyesia alikuwa mtoto wa kwanza wa mke mkubwa. Nsero alikataa kubatizwa kwa madai kwamba haoni tofauti kati ya aliyebatizwa na asiyebatizwa.Mtoto wa mdogo wake Nsero anaitwa Nkanturu naye alikataa kubatizwa.

2).Ndoa .

Bibi Elikyesia Nsero Makileo alifunga ndoa na Elinewinga Nnyaka mwaka 1920.

3).Kubatizwa.

Bibi Elikyesia Makileo alibatizwa mwaka 1925 usharika wa Masama.

5).Vita ya Dunia.

Mwaka 1916 alikwenda vitani (vita kuu ya kwanza 1916-19). Wakati wanarudi toka vitani walitembea toka Posta-Dsm hadi Moshi Nyumbani, walianza safari watu 7 lakini walifika wawili naye akiwa mmoja wao, na alipofika akaoa bibi Elikyesia 1920.

Na kweli tumeona Bwana alimfanya kuwa mshindi kwelikweli,Haleluya! (Zab.60:12) .

Mzee Elinewinga Menda Nnyaka alimaliza safari yake mwaka 1984 akiwa na uzee mwema wa miaka 114 na rekodi bora kabisa (Nndumi Narumishwa Nde na Ma!) .

4. Elinewinga Maana yake nini.

Elinewinga maana yake ni Bwana alinifanya kuwa mshindi! Na kweli tumeona Bwana alimfanya kuwa mshindi kwelikweli,Haleluya! (Zab.60:12) Wanaoniheshimu nitawaheshimu na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu! (1 Sam.2:30 ).

.

Kwa hili kila mtu ajitafakari ni kivipi anamheshimu Bwana,utafiti wa haraka waonyesha wote waliomheshimu Bwana waliacha watu baada yao sio "Maraami"(angalia kila lilipofika kanisa na pale ambapo halikufika watu wake wakoje?).Kama unawapenda watoto wako jifunze kumheshimu Bwana naye atasimama na wanao Mwa. 26:2-5, Zab.112:2 (wazao wake watakuwa hodari) .

4a.Je Elinewinga alimheshimu Bwana?.

Yee Mmbee!Mwaka 1922 Alishirikiana na Hayati Mwl. Zakaria Swai (Babake na Veraeli Swai) pamoja na watu wengine wa Lukani kuanzisha nyumba ya sala Lukani. Baadae hii nyumba ya sala ilikuja kuzaa usharika wa Lukani ambapo alikuja kuchaguliwa kuwa mzee wa kanisa.

Kweli tunaona huyu babu amekuwa Eli newinga kwelikweli (Bwana amemfanya mshindi) amelitendea haki hili jina na wazao wake wamekuwa hodari duniani.

6).Bibi Elikyesia Katokea wapi?.

6a) Watoto wa Salema -Elianshitaua,Nsero,Ndesamburo

6b) Watoto wa Elianshitaua- Alesikwa,Veraumangi na Elfera

6c) Watoto wa Ndesamburo- Nkanturu,Shilewinga,Senyiaeli,Samiaeli,Onaeli,Shilekirwa,Ndumaeli(mke wa Fitakyasa),Shisaeli,Kaeli,Anandumi,Veraeli,Apaisaria(aliolewa kwa Nderaguso),Elishekya,Zabuloni(Mwl. mstaafu alikaa Mtwara miaka mingi sana).

7).Bibi Elikyesia na ndugu zake.

Historia ya Bibi Elikyesia Makileo

Bibi Elikyesia Nsero alizaliwa mwaka 1890 akiwa mtoto wa kwanza wa Nsero. Bibi Elikyesia Nsero Makileo alifunga ndoa na Babu Elinewinga mwaka 1920 wakajaliwa kupata watoto 9

.
  • 1).Ndekirwa
  • 2).Ndelilio
  • 3).Isaeli
  • 4).Samwel
  • 5).Ndeshi
  • 6).Aseri
  • 7)Frank
  • 8).Magreth(Maika)

1).Bibi Nkangeresa

2).Nkangeresa aliishi Suumu, habari zake zaidi tutazipata kwa wanaomfahamu vizuri.

Nsero alikuwa na wake wawili . Watoto wa mke mkubwa ni Elikyesia, Salome(aliolewa Ng'uni kwa Anamwikira mtoto wao anaitwa Sarieli ambaye mke wake aliwahi kuwa mbunge), mtoto mwingine wa Nsero ni Nkangeresa(Huyu aliolewa huko Kashashi), anayefuata ni Elia(Baba yake Elisaa, David na Askari mstaafu anayeishi Sanya juu), toka Elia anayefuata ni Abraham wa Masaini(watoto wake ni Festo na Veraufoo)..

3.Elia

Elia Nsero huyu kwake ni pale Nkwatuke watoto wake ni David (Baba yake Idd Amini), Elisaa, na wengine

Watoto wa Ndesamburo (kwa mama mkubwa) -Nkanturu(ndo mtoto wa kwanza alizaliwa 1902 hakubatizwa naye kama Nsero), Shilewinga, Senjiaeli, Samiael(Baba yake Samson Kileo),Mwl. Onael, Shilekirwa(Magazeti), na Ndumaeli (mke wa Fitakyasa Natai)

.

4).Abraham

Abraham ni mdogo yake bibi aliishi kule Masaini.

Watoto wa Ndesamburo (kwa mama mdogo)- Shisaeli(baba yake na Terevaeli), Kaeli, Anandumi,Veraeli, Apaisaria(aliolewa kwa Nderaguso) mamaake na Shaftaeli na Ndesamburo, Elishekya,........, na Zabuloni (Mwalimu mstaafu alikaa Mtwara miaka mingi

5).Daniel

Huyu Daniel ni mdogo yake Bibi Elikyesia lakini mama tofauti, huyu Danieli ni Mzaliwa wa kwanza kwa mama mdogo na bibi ni mzaliwa wa kwanza kwa mama mkubwa

Nsero

Watoto wa Nsero(mama mdogo) - Daniel (Kwake ni Sufi njia ya kutokea Yuri), Reuben Kileo (Baba yake Jesmat), Bariki (kwake ni Nkwatuke),Elipokea (alikuwa meneja wa TANESCO Mafia, Baada ya Elipokea walizaliwa wanawake wawili (majina sikumbuki) mmoja aliolewa kwa Munuo huko Ng'uni, na mwingine aliolewa Mashua inasemekana mme wake alipata kichaa

7). Elinewinga na Uongozi.

Mwaka 1936 mzee Elinewinga Nnyaka alichaguliwa kuwa 'Nshili' (Kiongozi) wa Lukani na Ng'uni na baadae aliongezewa eneeo la Kyuu. Akiwa 'Nshili' alishawishi wananchi wa Lukani,Ng'uni na Kyuu kushika mashamba na kulima katika maeneo ya Yuri,Sufi na Lawate ambayo yalikuwa mapori. Yeye mwenyewe alionyesha mfano kwa kushika mashamba ya kutosha ambayo mpaka leo wajukuu wengi wamemilikishwa ! Akiwa Nshili wa Maeneo haya alifungua barabara za mitaa yote ya maeneo hayo! Vile vile alichaguliwa kuwa Bwana shamba wa eneo lote la Masama.

Elinewinga hakuwa kwenye familia ya utawala kwa yeye kupewa 'ushili' . Huu uongozi aliupata baada ya 'Nshili' aliyekuwepo kupoteza kodi(Hawa viongozi ndio waliokuwa wanasimamia kodi ktk maeneo yao, na hapa tuna ona Ndelimo akipoteza nafasi yake ya uongozi na kuchukuliwa na Elinewinga. Ndelimo alikuwa kabla ya Elinewinga.