Elinewinga Family
img img

1).Eliombera - Kuzaliwa.

Eliombera Sindaeli alizaliwa mwaka 19 . Eliombera ni dada yake na mama yake mke wa Aseri Elinewinga ( Bibi yake na Disraeli Aseri) . Kwa kifupi Baba mdogo Rowland ni Mjomba wake Disraeli na ni Baba mdogo wake Disraeli

2).Eliombera - Kubatizwa.

.

Mama Eliombera alibatizwa mwaka 1935 usharika wa Masama.

2).NATAI - HISTORY BACKGROUND.

image

Na kweli tumeona Bwana alimfanya kuwa mshindi kwelikweli,Haleluya! (Zab.60:12) .

Mzee Elinewinga Menda Nnyaka alimaliza safari yake mwaka 1984 akiwa na uzee mwema wa miaka 114 na rekodi bora kabisa (Nndumi Narumishwa Nde na Ma!) .

3. Elinewinga Maana yake nini.

Elinewinga maana yake ni Bwana alinifanya kuwa mshindi! Na kweli tumeona Bwana alimfanya kuwa mshindi kwelikweli,Haleluya! (Zab.60:12) Wanaoniheshimu nitawaheshimu na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu! (1 Sam.2:30 ).

.

Kwa hili kila mtu ajitafakari ni kivipi anamheshimu Bwana,utafiti wa haraka waonyesha wote waliomheshimu Bwana waliacha watu baada yao sio "Maraami"(angalia kila lilipofika kanisa na pale ambapo halikufika watu wake wakoje?).Kama unawapenda watoto wako jifunze kumheshimu Bwana naye atasimama na wanao Mwa. 26:2-5, Zab.112:2 (wazao wake watakuwa hodari) .

4.Je Elinewinga alimheshimu Bwana?.

Ndio, Mwaka 1922 Alishirikiana na Hayati Mwl. Zakaria Swai (Babake na Veraeli Swai) pamoja na watu wengine wa Lukani kuanzisha nyumba ya sala Lukani. Baadae hii nyumba ya sala ilikuja kuzaa usharika wa Lukani ambapo alikuja kuchaguliwa kuwa mzee wa kanisa.

5).Watoto NATAI

ONDUMAI .

NATAI .

UNGESI .

a) Nange b)Natai.

a1)Nsariko b1). Marang'a .

a1i).Ulomi...a1ii).Meturumu...a1iii)Nnyaka...a1iv).Meenda...a1v).Elinewinga .

a2i).Makaro...a2ii).Ruwele..a2iii).Salema...a2iv).Kirenga...a2v).Rundyaeli .

b1.Natai....b2.Marang'a....b3.Ntele....b4.Nkyeyo....b5.Kikoka....b6.Mantiri....b7.Omari...b8.Hoseya.

.Watoto wa Sindaeli.

i).Elilia

Elilia - Mtoto wa pili wa Sindaeli, makazi yake ni Yuri chini ya kwa Robert .

Grace Family

ii.Elianshisaria

Elianshisaria - Huyu nyumbani kwake ni Kirongoni ni baba yake na Hilife .

Allen Allen

iii.Elieshi Nlula

Elieshi Nlula- Aliolewa na mdogo wake na mwalimu Nlula pale Kashashi jirani na Alexander Itael .

Uongozi Elinewinga

iv.Ananndumi

Ananndumii - Huyu naye alibaki Kirongoni ANANNDUMI .

Terevaeli - Huyu ni Medical Doctor amekuwa akifanya kazi hospitali mbalimbali mara ya mwisho alikuwa hospitali moja pale Bomang'ombe

Ngao Elinewinga

v.Elikarisa

Elikarisa - Huyu aliolewa kwa Elfasi Ngunda hapo Mungomae (Ni mama yake na mama yake Disra).

Dora Family

vi.Eliombera

Angali Historia ya Eliombera

Grace Family

5).Watoto wa Sindaeli

vii.Ndeshifwaya - Huyu makazi yake ni Lemira (watoto wake walikuwa na duka Moshi mjini double road.

.

viii.Eliakundi - Huyu alikuwa Mhandisi huko Shinyanga ameshastaafu amerudi nyumbani.

6). Elinewinga na Uongozi.

Mwaka 1936 mzee Elinewinga Nnyaka alichaguliwa kuwa 'Nshili' (Kiongozi) wa Lukani na Ng'uni na baadae aliongezewa eneeo la Kyuu. Akiwa 'Nshili' alishawishi wananchi wa Lukani,Ng'uni na Kyuu kushika mashamba na kulima katika maeneo ya Yuri,Sufi na Lawate ambayo yalikuwa mapori. Yeye mwenyewe alionyesha mfano kwa kushika mashamba ya kutosha ambayo mpaka leo wajukuu wengi wamemilikishwa ! Akiwa Nshili wa Maeneo haya alifungua barabara za mitaa yote ya maeneo hayo! Vile vile alichaguliwa kuwa Bwana shamba wa eneo lote la Masama.

Elinewinga hakuwa kwenye familia ya utawala kwa yeye kupewa 'ushili' . Huu uongozi aliupata baada ya 'Nshili' aliyekuwepo kupoteza kodi(Hawa viongozi ndio waliokuwa wanasimamia kodi ktk maeneo yao, na hapa tuna ona Ndelimo akipoteza nafasi yake ya uongozi na kuchukuliwa na Elinewinga. Ndelimo alikuwa kabla ya Elinewinga.