1.Kuzaliwa -Mzee Elinewinga
Elinewinga Menda Nnyaka alizaliwa wakati wa Ifumu lya Saiye hii ni kabla ya 1871.Alizaliwa Nkwantana kijiji cha Ng'uni. Walihama kutoka Ng'uni kwenda Lukani mpakani -Forest, baadae walihama hapo na kwenda kuishi Kisawe (Kisawe ni pale kwa Amani wa Zebedayo). Walihama tena hapo Kisawe na kwenda Urereny na baadae kabisa walihamia Nkumbi ambapo ndipo alipoishi maisha yake yote hakuhama tena .2.Mzee Elinewinga apigana vita kuu ya Dunia.
Mwaka 1916 alikwenda vitani (vita kuu ya kwanza ya Dunia 1916-19). Wakati wanarudi toka vitani walitembea toka Posta-Dsm hadi Moshi Nyumbani, walianza safari watu 7 lakini walifika wawili naye akiwa mmoja wao.Na kweli tumeona Bwana alimfanya kuwa mshindi kwelikweli,Haleluya! (Zab.60:12) .
Mzee Elinewinga Menda Nnyaka alimaliza safari yake mwaka 1984 akiwa na uzee mwema wa miaka 114 na rekodi bora kabisa (Nndumi Narumishwa Nde na Ma!) .
3. Elinewinga Maana yake nini.
Elinewinga maana yake ni Bwana alinifanya kuwa mshindi! Na kweli tumeona Bwana alimfanya kuwa mshindi kwelikweli,Haleluya! (Zab.60:12) Wanaoniheshimu nitawaheshimu na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu! (1 Sam.2:30 ).
.Kwa hili kila mtu ajitafakari ni kivipi anamheshimu Bwana,utafiti wa haraka waonyesha wote waliomheshimu Bwana waliacha watu baada yao sio "Maraami"(angalia kila lilipofika kanisa na pale ambapo halikufika watu wake wakoje?).Kama unawapenda watoto wako jifunze kumheshimu Bwana naye atasimama na wanao Mwa. 26:2-5, Zab.112:2 (wazao wake watakuwa hodari) .
5. Elinewinga achaguliwa kuwa Kiongozi wa Serikali(Nshili).
Mwaka 1936 mzee Elinewinga Nnyaka alichaguliwa kuwa 'Nshili' (Kiongozi) wa Lukani na Ng'uni na baadae aliongezewa eneeo la Kyuu. Akiwa 'Nshili' alishawishi wananchi wa Lukani,Ng'uni na Kyuu kushika mashamba na kulima katika maeneo ya Yuri,Sufi na Lawate ambayo yalikuwa mapori. Yeye mwenyewe alionyesha mfano kwa kushika mashamba ya kutosha ambayo mpaka leo wajukuu wengi wamemilikishwa ! Akiwa Nshili wa Maeneo haya alifungua barabara za mitaa yote ya maeneo hayo! Vile vile alichaguliwa kuwa Bwana shamba wa eneo lote la Masama.WATOTO WA MEENDA.
1. Elineshikwa Meenda.
2.NDESAMBURO MEENDA.
1.Unike mke wa Uliki
2.Zebedayo
3.Shangazi wa Kibosho Kombo- aliolewa kule 1954
4.Shangazi wa Kyuu- pale shule ya msingi
5.Irine
6.Beliam
7.Dausen
8.ApaaUrilal
3.MANGATARI.
Aseri Family
4.SHITIRINSIANDE.
Elinewinga Family
.....
5.MAMKWE.