1.) Ndesamburo .

Ndesamburo Menda Nnyaka ni nani na aliishi wapi?.

Ndesamburo ni mdogo wake Babu Elinewinga.Huyu ni Baba yake na Boronga, ni Babu yake na Amani wa Zebedayo.Ndesamburo alifariki kitambo kidogo wajukuu wengi hawakumfahamu ila mke wake ndiye wengi tulimkuta. Mke wake Ndesamburo aliitwa (Makitika).Makitika alikuwa maarufu bale urereny kwa kilimo cha mahindi ya mapema kuliko watu wengine wote.Kila Chrismass ya kila mwaka pale kwa bibi makitika utapata mahindi mabichi ya kuchoma, mlimani bado, baada ya huyu bibi kuondoka mahindi pale hakuna tena.Bibi Makitika alifariki miaka ya elfu mbili akiwa na miaka 120. .

Mzee Ndesamburo aliishi pale Urereny mahali alipokuwa akiishi Menda.

2). Watoto wa Mzee Ndesamburo na mahali walikoishi.

1. Eunike Ndesamburo

Eunike aliolewa na mtu wa Lyamungo mzee Uliki , Babu akawapatia sehemu (kyamba) pale Nkwatuke wakaja kujenga pale hata leo. Huyu Eunike , mtoto wa Ndesamburo alijaliwa watoto wanne (4) , wa kwanza ni Angasiriny(alizaliwa 1943) na wa mwisho ni Ndenfoo 'Mabangi' (Huyu akizaliwa 1950). Mke wa Estomih Swai pale Losaa ni mtoto wa Unike.Estomih Swai ni miongoni mwa majirani wa mzee wetu Isaeli pale Losaa kwa sasa Adam. Hii ni kusema kuwa huyu mke wa Estomih Swai ni Mjukuu mwenzetu.

Na kweli tumeona Bwana alimfanya kuwa mshindi kwelikweli,Haleluya! (Zab.60:12) .

Mzee Elinewinga Menda Nnyaka alimaliza safari yake mwaka 1984 akiwa na uzee mwema wa miaka 114 na rekodi bora kabisa (Nndumi Narumishwa Nde na Ma!) .

Elinewinga Maana yake nini.

Elinewinga- Elinewinga maana yake ni Bwana
alinifanya kuwa mshindi!

Na kweli tumeona Bwana alimfanya kuwa mshindi kwelikweli,Haleluya! (Zab.60:12) .

Wanaoniheshimu nitawaheshimu na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu! (1 Sam.2:30 ).

Kwa hili kila mtu ajitafakari ni kivipi anamheshimu Bwana,utafiti wa haraka waonyesha wote waliomheshimu Bwana waliacha watu baada yao sio "Marami"(angalia kila lilipofika kanisa na pale ambapo halikufika watu wake wakoje?).Kama unawapenda watoto wako jifunze kumheshimu Bwana naye atasimama na wanao Mwanzo 26:2-5 .

2.Zebedayo Ndesamburo.

Zebedayo Ndesamburo Menda Nyaka ni mtoto wa kwanza wa kiume, huyu aliishi pale anakoishi mtoto wake(Amani). Mke wa Zebedayo aliitwa 'AlewiriyoMuu'(aliyefufuliwa kwa wasiojua kichaga) alifariki juzi juzi, Zebedayo yeye alifariki miaka ya 70, Pamoja na Amani, Zebedayo alikuwa na watoto kadhaa wa kike akiwepo mke wa Makalla, mwingine aliolewa Iringa wanaishi Shekilango, mwingine aliolewa hapo Forest karibu na anakoishi mtoto wa John Gabriel(Kifisi), toka kwa Isaack ni kwa 'kifisi'

3. Travinesi Ndesamburo.

Travinesi ni mtoto wa nne wa Ndesamburo Menda, mtoto wa tatu manka alifariki. Huyu Shangazi Travinesi aliolewa kwa Mboya pale Kibosho maeneo ya Kombo ndiko wanaishi, alikuwa na kijana anaitwa Imanu ,pamoja naye kuna wengine akiwepo dada ambaye anaishi Dar es Salaam kwa muda mrefu sasa

4.Irene Ndesamburo.

Irene. - Huyu aliishi pale Forest , alikuwa na Watoto watatu - Samweli (Talu), na Madikoo

5.Apaa Urilaly Ndesamburo

Apaa Urilaly- Aliishi Kenya siku nyingi baadae alirudi nyumbani kumtunza mama yake. Alikuwa na mtoto wake kwa jina Riziki

6. Beliam Ndesamburo.

Huyu Beliam alifariki zamani kidogo watu wengi wa Lukani hawakumfahamu alikaa sana huko West Kilimanjaro akijishughulisha na kilimo. Aliacha watoto wawili mmoja ni Lameck mwingine alifariki miaka ya karibuni.

7.Ester Ndesamburo.

Ester Ndesamburo - aliolewa kule Kyuu jirani kabisa na shule ya Kyuu ,pamoja na wengine ana kijana anaitwa Stanley

8. Dausen Ndesamburo (Boronga).

Dausen- Huyu ni wa mwisho na aliweka makao yake hapo kwa Baba yake , alijulikana mtaani kwa jina la Boronga

Historia ya Eunike Ndesamburo.